ALAMA ZA NYAYO ZA MIGUU YAKO
Alama za nyayo za migugu yako hazifanani na alama za nyayo za miguu ya mtu mwingine yeyote yule. Kila unakoelekea alama za nyayo zako, hukufuata nyuma yako na wala huwezi kuzifuta au kuzizuia zisikufuate. Mahali ambapo miguu yako imekanyaga, hakuna mtu mwingine anayeweza kukanyaga alama za nyayo za maisha yako. Kila mtu Mungu kampangia maisha yake ambayo hayafanani na maisha ya mtu mwingine, kama zilivyo alama za nyayo za miguu yetu.
Mwisho wa safari yetu ya hapa duniani ndio mwanzo wa safari yetu ya mbinguni; duniani tunapita. Alama nzuri au mbaya ya maisha yetu, itabaki siku zote nyuma yetu kama vile nyayo za miguu ziachavyo alama nyuma yetu.Tusikubali tufikie mwisho wa safari yetu bila ya kuacha alama iliyo nzuri ya maisha yetu. Kazi zetu, matendo yetu na maisha yetu, yaache alama itakayokumbukwa.
Yesu anasema, “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.” (Ufunuo 22:12-13)