Skip to Content

MAISHA NI ZAWADI

6 Januari 2026 na
MAISHA NI ZAWADI
Sr. Violet Kwanungu LSOF
| Hakuna maoni bado

MAISHA NI ZAWADI

Maisha ni zawadi nzuri aliyotujalia Mwenyezi Mungu ni zawadi ambayo hatuwezi kuipata mahali pengine popote pale. Uhai wa maisha yetu, ni zawadi isiyoweza kununulika kwa ghalama zozote zile, tuitunze zawadi yetu. Maisha ni ya thamani kubwa ni vema kuyathamini, tuishi vizuri hapa duniani kwani sisi sote ni ndugu tujaliwe kupata baraka za Mwenyezi Mungu.

“Kwa sababu hiyo nawaambieni: msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je, si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je, si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo: hayafanyi kazi, wala hayasokoti. Nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema: tule nini? Au tuvae nini?  Kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho, kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.” (Mathayo 6: 25-34)

katika Blog yetu
MAISHA NI ZAWADI
Sr. Violet Kwanungu LSOF 6 Januari 2026
Shiriki posti hii
Madaraka
Sign in to leave a comment