Matangazo ya Parokia
Tunawashukuru sana jumuiya ya Mt. Martin wa Pores waliosafisha Kanisa jana. Idadi yao ni 12. Wiki ijayo ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Polycarp wakifuatiwa naJumuiya ya Mt. Hyasinta.
Mafundisho ya Komunio ya Kwanza na Kipaimara kwa lugha ya Kiingereza yataanza Jumamosi ijayo tarehe 24/01/2026. Siku za mafundisho ni kila Jumamosi na Jumapili. Saa 02:00 asubuhi Mpaka 04:00.
Baba Paroko atakuwa na kikao na Wenyeviti na Watunza Fedha wa Kanda zote 8 Dominika ya tarehe 25/01/2026 mara baada ya Misa ya pili Kwenye darasa la Mikutano. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria wito huo wa Baba Paroko bila kukosa. Aidha, kila Kanda itawasilisha kwake siku hiyo ratiba ya Misa za Kanda kwa mwaka mzima wa 2026.
Baba Paroko ameanza tena ziara za Kichungaji za kubariki nyumba za Wana Parokia ambazo hazikuwa zimefikiwa. Kwa wahusika tunaombwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa jumuiya na Kanda ili Paroko aweze kuhitimisha zoezi hili kwa awamu hii.
Kwaya ya Moyo Mt wa Yesu ya hapa Parokiani, watazindua album ya nyimbo katika picha mjongeo(video) siku ya tar. 15/02/2026 kuanzia saa kumi kamili jioni.
Tiketi zinapatikana nje ya kanisa kwa bei zifuatazo:
TZS30,000
TZS50,000
TZS100,000(VIP)
Meza ya VIP kwawatu 10kwaTZS 1,000,000
Karibuni tuwaunge mkono katika uinjilishaji.
MATANGAZO YA NDOA
TANGAZO LA KWANZA
Charles Beatus Mbunda na Bertina Daniel Mpachoka
Wilfred Ambokile Mapunda na Helena Agnel Nalinga
Gabriel Edward Mliga na Carolina Gerald Nyasingo
Gilbert Abel Munishi na Anastazia Ambrose Njau
Jackson Lucas Hugo na Joyce Ali
Deokary Dia Msigwa na Adorofina William