1.Tunawashukuru sana Jumuiya ya Mt.LeoMkuu waliosafisha Kanisa jana. Idadi yao ni 14 Wiki ijayo ni zamu ya jumuiya ya Mt.LukaMwinjili watafuatiwa na Jumuiya ya Mt.BikiraMariaMlimawaKarmel.
2.Jumuiya ambazo hazijawasilisha michango ya2000/= kwa kila mbatizwa kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa Kuu Mbadala Pugu zinaombwa kukamilisha zoezi hilo. Hali kadhalika wenyeviti wa Jumuiya mnaombwa kuwasilisha orodha ya waamini waliochangia michango hiyo kwa aajili ya kuweka kumbukumbu vizuri.
3.Baba Askofu Mkuu Mhashamu sana Jude Thadeus Ruwaiichi ameandaa chakula cha Hisani kwa ajili ya Tegemeza Kanisa. Askofu Mkuu anatualika wote kushiriki na kumuunga Mkono katika jukumu hilo la kuwezesha ukuaji wa Utume wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa kununua kadi ambazo zinauzwa nje ya Milango ya Kanisa. Karibu wote kwa umoja wetu wa Kiparokia kumuunga mkono.
Sote tunakaribishwa kwa moyo mkunjufu kuja pamoja kama jumuiya ya parokia na kusaidia juhudi hii muhimu.
4.Kutakuwepo na Mkutano Mkuu wa vijana Dominika ya tarehe 20/09 katika moja ya Madaraasa mara baada ya Misa ya saa 5:15. Vijana wote mnaalikwa kuhudhuria bila kukosa.
5.Idara ya Kichungaji ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam inatualika Waamini wote wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kushiriki Wsrsha maalum itakayofanyika tarehe 26 Septemba, 2026 katika Uwanja wa Uhuru.Lengo la Warsha hizi ni kutuimarisha kiimani na kujenga umoja wa Kisinodi Jimboni kwetu.
Aidha,tunaombwa kuchangia ada ya ushiriki ya shilingi 5,000 ambayo itatumika kulipia gharama mbalimbali.Tujiandikishe kupitia Jumuiya zetu.
6.Tunapenda kuwakumbusha kuendelea kulipa ahadi za Tegemeza Kanisa kwani kilele cha zoezi hilo kwa mwaka huu kimekaribia sana.
7. TANGAZO LA PILI LA UPADRE - SHIRIKA LA MATESO YA YESU KRISTO
Diakoni Richard Seraphine Mlay
KutokaParokia ya Chang’ombe
8.Mtu yeyote anayejua kuhusu kikwazo chochote anakaribishwa kutoa taarifa kwaPadri wa Parokia. Zaidi ya yote, tuwe na kumbukumbu yake katika maombi yetu.
MATANGAZO YA NDOA
TANGAZO LA II
- Anthony Joel Birope na Martha Adam Luhanga
- Andrew Akilei Macha na Rose Anthony Ndauka
- Juvenal Ladislaus Kimaro na Neema Paulo Urio
- James Donald Davisen na Rose Anthony Joachim
TANGAZO LA III
- Oscar Novatus Mbelwa na Rachel Anthony Njawike
ASANTE SANA KWA WEMA WENU. MUNGU AWABARIKI NYOTE. 🙏✝️